MWANAFUNZI BORA KIDATO CHA NNE AWATAKA VIONGOZI WAWE WAKWELI, WAADILIFU

Nyakaho Marungu akiwa kwenye pozi.
…Akiwa na binamu yake.
Mama mzazi wa Nyakaho, Celestina Maro (kushoto),  akiwa na baba yake mdogo, Emmanuel Mgaya.
Mwandishi wa tovuti na TV Online wa GPL (katikati) akitoa pongeza  kwa mama yake Nyakaho.
MSICHANA Nyakaho Marungu (16) mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Baobab, mkoani Pwani aliyeibuka mwanafunzi bora wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014 nchini, amewataka viongozi  nchini kuwa wakweli na waadilifu ili kuiletea nchi maendeleo na kutokumuudhi  Mwenyezi Mungu.
Akizungumza na GPL nyumbani kwao Kitunda, jijini Dar es Salaam, amesema  wanafunzi wanaofanya vizuri wako wengi, ila hawapatiwi nafasi ya kuendelezwa taaluma zao. Aidha msichana huyo ametoa ushauri kwa wanafunzi kutenga muda wa kusoma kwa bidii na muda  wa kupumzika huku wakimtegemea Mungu.

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII

Previous
Next Post »
Thanks for your comment