Joseph Kusaga: Clouds FM haina chama! Akanusha Clouds kununuliwa na Rostam Aziz


Clouds fm wamekana kuwa shutuma zinazotolewa kwenye social media hasa jamiiforums kwamba wao CCM sio za kweli.

Akihojiwa CEO wa clouds katika kipindi power breakfast, amesema wao kama radio hawana chama kwa sababu hata sheria TCRA haziruhusu.

Pia kwenye uchaguzi wa mwaka huu wagombea wote watapewa nafasi sawa.

Ameendelea kusema kuwa wafanyakazi wachache kuwa CCM haimaanishi clouds yote ni CCM.

Pia clouds imekanusha habari zilizozagaa kuwa radio imenunuliwa na Rostam Aziz, ameongeza kuwa hizo ni propaganda za kuichafua radio hiyo.

Amesema kama wakiuza radio watatangaza kwasababu radio ni yao,na hawamuogopi mtu.

Wakati wanamuhoji nimesikia wanamuita Joh (labda ndiye Joseph Kusaga) sina uhakika na majina mengine,wanomfahamu watatujuza.

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII

Previous
Next Post »
Thanks for your comment