Luckey: Wasanii Wakubwa Wanabebwa na Mavazi

MWIGIZAJI na muongozaji wa filamu Bongo Luckey Luckamo amewashukia wasanii wakubwa kuwa uwezo wao wa kuigiza ni mdogo sana lakini baadhi ya watayarishaji wanawapenda kwa sababu ya mavazi yao katika filamu kitu kinachosaidia kupunguza gharama kwao lakini kiwango chao ni kidogo sana.
“Katika tasnia ya filamu kuna changamoto nyingi, lakini ngumu kuliko yote ukikutana na filamu inayoshirikisha wasanii Nyota, tatizo kwani wengi wao uwezo wao upo chini sana, lakini wanabebwa na mavazi tu kwa sababu wapo nadhifu,”anasema Luckey.
Msanii huyo anasema kuwa kama si watayarishaji kutawaliwa na mawazo ya kuamini kuwa wasanii wakubwa ndio wanaouza basi wasanii wakubwa wangekuwa wamepotea na soko la filamu kutawaliwa na wasanii wenyewe uwezo na si majina kama ilivyo sasa, ambapo wasanii wazuri hawapewi nafasi.
Mwanaspoti

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII

Previous
Next Post »
Thanks for your comment