MAASKARI WA BODABODA

Askari polisi wa doria ya pikipiki maarufu kama tigo wakiongea  na kijana aliyekuwa akiendesha pikipiki na mtu aliyempakiza.
Wakiendelea kuongea nao.
Askari polisi wa doria ya pikipiki maarufu kama tigo, mwishoni mwa wiki iliyopita walimfanyia jambo baya kijana aliyekuwa akiendesha pikipiki na mtu aliyempakiza kwa kuikamata na kuibinua juu na kuwabwaga kwenye lami.
Kitendo hicho kilizua hasira kwa jamaa aliyepakizwa ambapo aliwavaa askari hao kwa kuwatolea maneno makali. Jamaa alipozidi kutoa maneno yaliyowakera askari hao afande mmoja alimnyooshea bunduki na kutaka kumfyatulia.
Hata hivyo baada ya muda mfupi raia walioshuhudia tukio hilo waliwazingira askari hao na kuwaeleza kuwa walifanya kitendo kisicho cha kiungwana kwa mwendesha pikipiki huyo na abiria wake.
Imedaiwa kuwa eti maafande hao shida yao ilikuwa kutaka kumkagua dereva huyo kama ana leseni ya udereva, bima ya pikipiki aliyokuwa akiendesha na kosa la kutovaa kofia.
Angalia picha.   

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII

Previous
Next Post »
Thanks for your comment